
Nyota wa muziki nchini Uganda Bebe Cool amewashauri waandishi wa nyimbo nchini humo kuelekeza nguvu zao kwenye suala la kuandika nyimbo badala ya kujilazimisha kuwa waimbaji.
Kwenye mahojiano na runinga moja nchini Uganda Bebe Cool amesema ni vigumu kwa msanii kufanya kazi mbili kwa wakati mmoja kwenye tasnia ya muziki kwani mwisho wa siku moja humpokonya.
Ikumbukwe Bebe Cool hajakuwa na uhusiano mzuri na waandishi wa nyimbo nchini uganda ikizingatiwa kuwa ana kesi mahakamani iliyowasilishwa na Black Skin ambaye alidai kuwa licha kumuandikia msanii huyo wimbo wake wa “Gyenvude alidinda kumlipa pesa zake.