
Baada ya kusainiwa na lebo ya sony Entertainment Group msanii kutoka nchini Uganda Vinka alipunguza idadi ya nyimbo alizokuwa anatoa kwa mashabiki zake.
Msanii huyo wa Swangz Avenue aliachia nyimbo tatu mwaka wa 2021 ambazo ni Thank God, Loving akiwa amemshirikisha Roberto na Kimuli Kyange aliyoshirikishwa na Mudra.
Sasa akiwa kwenye mahojiano na NBS TV Vinka aliwashangaza wadau wa muziki nchini Uganda baada kutaja majina ya nyimbo zake mbili na akapata kigugumizi kutaja jina la wimbo wake wa tatu ambao ni Loving.
Jambo hilo lilimfanya Vinka kuwaomba mashabiki zake msamaha kwa kitendo cha kusahau jina la wimbo wake wa tatu akiwa hewani baada ya mtangazaji wa kituo cha runinga cha NBS kumkumbusha jina la wimbo huo.