Entertainment

JACKIE CHANDIRU: WAGANDA WANA ROHO CHAFU,WALINITUSI HADI NIKAHAMIA KENYA

JACKIE CHANDIRU: WAGANDA WANA ROHO CHAFU,WALINITUSI HADI NIKAHAMIA KENYA

Aliyekuwa msanii wa kundi la Blue 3 kutoka Uganda Jackie Chandiru amefunguka juu ya changamoto alizokutana nazo wakati alikuwa ameathirika na uraibu wa dawa za kulevya.

Katika mahojiano yake ya hivi karibuni, Chandiru amesema Waganda hawakumpa muda wa kupona kutoka kwa uraibu wa mihadarati kwani kila mara walikuwa wanamkosoa badala ya kumpa msaada.

Hitmaker huyo wa “Gold Digger amesema kipindi picha zake zilifuja mtandaoni akiwa hali mbaya, alipokea matusi ya kila aina kutoka kwa Waganda jambo ambalo anadai lilimlazimu kutimkia nchini Kenya.

“Waganda hawakunipa nafasi ya kupona, walipoona picha zangu nikiwa katika hali ya kutisha, walinitusi, na hali yangu ikawa mbaya zaidi. Ndio maana nimekaa muda mwingi nchini Kenya,” alisema.

Chandiru hata hivyo anasema ataendelea kuishukuru familia yake na marafiki ambao walifanya kila wawezalo kumuona akifurahia maisha tena.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *