Entertainment

LIL DUVAL AKERWA NA KITENDO CHA WANAWAKE MAREKANI KUWABAMBIKIA KESI ZA UBAKAJI BAADHI YA WANAUME

LIL DUVAL AKERWA NA KITENDO CHA WANAWAKE MAREKANI KUWABAMBIKIA KESI ZA UBAKAJI BAADHI YA WANAUME

Mchekeshaji Lil Duval kutoka nchini Marekani, ameonesha kukerwa na kitendo cha baadhi ya wanawake kuwabambikia kesi za ubakaji baadhi ya wanaume maarufu nchini humo.

Duval amesema hayo huku akitolea mfano sakata la sasa lililomkuta Chris Brown, akishutumiwa kumbaka mwanamke mmoja ambaye hakutajwa jina huku baadhi ya taarifa na ushahidi zikimuonesha mwanamke huyo, akimuomba Chris kufanya nae tendo la ndoa kwa hiyari.

Mchekeshaji huyo amesisitiza kuwa anatamani kuona siku moja wanawake wakiwajibishwa kwa kutoa tuhuma za uongo dhidi ya wanaume, ili kukomesha vitendo hivyo ambavyo vinazidi kuongezeka kwa kasi nchini Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *