
Staa wa Bongofleva, Diamond Platnumz huwenda yupo mbioni kufunga ndoa mara baada uvumi wa zaidi ya miaka miwili.
Hiyo ni baada ya mama yake mzazi, Bi. Sandraa maarufu kama Mama Dangote kudokeza kuwa mwimbaji huyo amempata mwenza.
“Nashindwa kuelezea furaha yangu mwanangu, Naseeb (Diamond Platnumz) hapa sasa umepata mwenza, utulie Baba yangu uoe,” amesema Mama Dangote kupitia Instagram.
Utakumbuka toka Aprili 2020 Diamond alipoachana na mpenzi wake toka nchini Kenya, Tanasha Donna hajawahi kuweka wazi mahusiano yake.