
Msanii na prodyuza wa muziki nchini Uganda Kalifah Aganaga ametia nia ya kugombea wadhifu wa unaibu wa rais katika muungano wa wanamuziki nchihi humo kwenye uchaguzi wa mwaka huu
Kupitia mitandao yake ya kijamii Aganaga amesema ana vigezo vyote vya kuwa naibu wa rais wa muungano huo ikizingatiwa kuwa ana uelewa mpana wa changamoto zinazowakumba wanamuziki nchini uganda.
Hata hivyo ametoa wito kwa wanachama wa UMA kuunga mkono azma yake ya kuwa naibu wa rais wa muungano huo huku akiwataka wampe kura zao, uchaguzi wa kuwachagua viongozi wapya utakapowadia.