Entertainment

FAT JOE ATANGAZA KUACHIA KITABU CHAKE

FAT JOE ATANGAZA KUACHIA KITABU CHAKE

Rapa mkongwe kutoka Marekani Fat Joe amethibitisha rasmi ujio wa kitabu chake kilichosheheni stori za maisha yake.

Kitabu hicho kinaitwa “The Book Of Jose” kitatoka rasmi Novemba 1, mwaka 2022 na amesimulia maisha yake kabla na baada ya kuwa msanii maarufu na tajiri dunia.

Kupitia video aliyochapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram Fat Joe amesema “Kuna stori kuhusu jinsi Fat Joe alivyotoka kwenye muziki, maisha ya umasikini aliyoishi, kupishana na kifo, alivyokuwa jela, kupoteza marafiki na jinsi alivyopambana na msongo wa mawazo”

Kitabu hicho kitakuwa kinapatikana katika mfumo wa sauti kama simulizi yenye video ili kuwarahisishia kazi  wale wanopendelea kusikiliza na kutazama picha zaidi kuliko kusoma vitabu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *