
Msanii wa muziki wa dancehalll kutoka Uganda Ziza Bafana amehapa kuanika maovu yote ambayo meneja wa Spice Diana, Roger Lubega alimfanyia kipindi wanafanya kazi pamoja.
Hii ni baada Gravity Omutujju kudai kwamba Spice Diana na meneja wake Roger Lubega ni wanafiki kwa kuwa hawajawahi watakia mema wasanii wengine kwenye shughuli zao za muziki.
Roger aliacha kufanya kazi na Ziza Bafana mwaka wa 2016 ambapo alianza kusimamia muziki wa Spice Diana baada ya msanii huyo kushindwa kumlipa pesa zake.
Tangu wakati huu Bafana amekuwa akisuasua kimuziki jambo ambalo limemfanya kumlaumu Roger Lubega kwa masaibu yanayomuandama huku akidai kuwa amemfanyia vitendo vya kishirikina.