
Msanii wa Bongofleva Loui anaendelea kufanya makubwa kupitia chati kubwa za Billboard Afrika Kusini.
Hitmaker huyo wa “Hennessy” amefikia hatua hiyo baada ya wimbo wao na mwimbaji Musa Keys kutoka Afrika Kusini, uitwao “Selema (Po Po)” kuendelea kusalia kwenye chati hiyo ukiwa nafasi ya 20 kwa nyimbo zinazofanya vizuri Afrika Kusini, wiki hii.
Kwa mujibu wa chart data tz wimbo huo umekaa kwenye chart hizo za Billboard kwa jumla ya wiki 13 na ulifanikiwa kushika nafasi za juu.
Utakumbuka, wimbo huo wa “Selema” pia umeshafikia kiwango cha mauzo ya PLATNUM kwa Afrika Kusini, hivyo unamfanya msanii Loui kuwa miongoni mwa wasanii wa Tanzania kufikia mafanikio hayo baada ya msanii Diamond Platnumz.