Entertainment

JAY Z AFUNGUKA KUSTAAFU MUZIKI

JAY Z AFUNGUKA KUSTAAFU MUZIKI

Rapa kutoka Marekani Jay-Z amefunguka kwamba hajastaafu kufanya muziki kama wengi wanavyodai.

Kwenye kipindi cha ‘Hart to Heart serie’ cha Mchekeshaji Kevin Hart amefunguka juu ya mipango yake aliokuwa nayo ya kutaka kustaafu Muziki.

“Nilijaribu hilo,” alisema kuhusu kustaafu kwake 2003. “Nilihitaji tu mapumziko. Nilikuwa nimechoka sana wakati huo. Nilikuwa nikitoa albamu kila mwaka… Nilitazama tu siku moja na nikasema, ‘Nimechoka.’ Sikuwahi kuwa likizoni hadi nilipotaka kusema 2000 — maisha yangu yote. Nilikuwa nimechoka sana wakati huo”- Alisema Jay Z.

Mbali na hilo Jay Z amezungumzia pia juu ya utoaji wake wa kazi kwa kipindi hiki na kusema kwamba hana mpango wa kuachia ngoma mpya hivi karibuni.

“Sifanyi muziki kwa bidii au kutengeneza albamu au kuwa na mipango ya kutengeneza albamu, lakini sitaki kamwe kusema kwamba nimestaafu,” alikiri. “Ni zawadi, kwa hiyo mimi ni nani wa kuifunga? Na inaweza kuwa na sura au tafsiri tofauti. Labda sio albamu, labda ni. Sijui, lakini nitawaacha wazi.”

Mara ya mwisho kwa Jay-Z kuachia album mpya ilikuwa mwaka 2017 ambapo aliiachia (4:44)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *