Entertainment

T.I ATUNUKIWA TUZO NA UONGOZI WA MJI WA GEORGIA

T.I ATUNUKIWA TUZO NA UONGOZI WA MJI WA GEORGIA

Rapa T.I. siku zote amekuwa akiuwakilisha vyema Mji wa Georgia kwenye Muziki wake na hata kuisadia Jamii ya watu wa mji huo. Kwa juhudi zake, Uongozi wa mji huo Jana ulimtunukia Tuzo ya heshima (Outstanding Georgia Citizen Award)

Akiongozana na familia yake, T.I. aliipokea heshima hiyo kwa mchango wake mkubwa ambao amekuwa akiutoa kupitia Taasisi yake, Harris Community Works. “Tupo hapa duniani kwenye haya maisha kwa muda mfupi na pindi tukiondoka, watu hawawezi kutukumbuka kwa mavazi tunayovaa, au vitu tunavyo miliki. Bali tutakumbukwa kwa tuliyofanya kwenye familia zetu, watoto wetu na kwa kile tuliweza kufanya kwa wengine.” alisema T.I.

Mbali na Tuzo hiyo, Rapa T.I. pia alikabidhiwa Tuzo ya ‘Volunteers Achievement Lifetime Award’ ambayo imetolewa na Global International Alliance kwa niaba ya Rais Joe Bidden, ikitoa heshima kwa masaa zaidi ya 4,000 ya kufanya kazi za Jamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *