
Rapa kutoka Marekani Blueface amepigwa ngumi ya uso na Girlfriend wake Chrisean Rock kwa mara nyingine tena.
Kwa mujibu wa TMZ, polisi walimtia pingu mrembo huyo na kumfikisha kituoni.
Huu umekuwa ni muendelezo wa vita baina yao, Agosti 3 mwaka huu wawili hao walitwangana na kunaswa kwenye video ya CCTV ambapo Blueface alisikika kwenye video akilalamika kukuta Rock anawasiliana na wanaume wengine kwenye simu, ikiashiria vitendo vya usaliti.