Entertainment

MSANII WA ZAMANI WA GRANDPA RECORDS MAJIRANI AAPA KUTOFILISIKA TENA KIUCHUMI

MSANII WA ZAMANI WA GRANDPA RECORDS MAJIRANI AAPA KUTOFILISIKA TENA KIUCHUMI

Aliyekuwa msanii wa Grandpa Records Majirani amehapa kutofulia kiuchumi tena kutokana na masaibu aliyokumbana nayo kipindi cha nyuma.

Msanii huyo ametoa ya moyoni kwa kusema kwamba umaskini ni kitu kibaya sana duniani huku akitupa kumbukumbu ya namna ambavyo mchumba wake alimkimbia licha ya kumtambulisha kwa wazazi wake kutokana na yeye kuyumba kiuchumi.

Hitmaker huyo wa “Tukumbukeko” ameenda mbali zaidi na kusema kuwa kilichomuumiza zaidi na kitendo cha mchumba yake huyo kumnyima tendo la ndoa kwa kipindi cha miezi mitano.

Utakumbuka mwaka 2021 majirani alijitokeza hadharani na kukiri kuwa anapitia wakati mgumu katika maisha yake ambapo aliwataka wakenya wamsaidie kifedha baada ya kufungiwa nyumba aliyokuwa akiishi kutokana na kushindwa kulipa kodi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *