
Staa mkongwe wa muziki wa rap nchini Tanzania, Professor Jay ameweka wazi kuachia EP mpya yenye jumla ya ngoma 5 hivi karibuni.
Kupitia ukurasa wake wa instagram Professa Jay ameandika ujumbe unaosomeka “Badala ya kuwapa chakula cha ubongo kwa single moja naona kama niwape chakula cha EP ya nyimbo 5 au mnasemaje Maboss wangu”
Professa Jay amebainisha hilo ikiwa ni takribani miezi 6 imepita tangu alipoachia hitsong yake iitwayo “Utanambia Nini”.