Mwanamuziki Hellen Lukoma amedai kuwa mjadala unaoendelea nchini Uganda wa kujaribu kuthibiti muziki wa Nigeria haumhusu ndewe wala sikio.
Kwenye mahojiano yake hivi karibuni msanii huyo amesema wanaijeria hautamzuia kuwapa mashabiki zake burudani huku akisisitiza kuwa ataendelea kutoa muziki mzuri ambao kwa njia moja au nyingine itamfungulia milango ikitokea ameenda tamasha lake mwenyewe.
Kauli ya Hellen Lukoma inakuja wakati huu baadhi ya wadau wa muziki nchini Uganda wanapendekeza kuwekwa kwa mikakati ambayo itawazuia mapromota kuwazingatia sana wasanii wa kigeni na badala yake wawape nafasi wasanii wa ndani kutumbuiza kwenye matamasha yao ya muziki.