Others

Rufftone afunguka sababu za kumchumbi mke wake kwa zaidi ya miaka 8

Rufftone afunguka sababu za kumchumbi mke wake kwa zaidi ya miaka 8

Msaniii mkongwe kwenye muziki nchini Rufftone amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu hatua ya kumchumbia mke wake Crystal kwa zaidi ya miaka 8.

Kwenye mahojiano na Plug TV rufftone amesema kipindi hicho alikuwa ameshikika na masuala ya muziki lakini pa alikuwa na marafiki wengi wa kiume kiasi cha kumfanya kusahau  kuingia kwenye maisha ya ndoa.

Hitmaker huyo wa “Mungu Baba” amesema aliogopa sana kuingia kwenye ndoa kwa sababu alikuwa anahisi mke angemnyima uhuru wa kutangamana na marafiki zake lakini baada ya kuhamua kuoa alikuja akagundua alipoteza muda mwingi kuwa na mitazamo hasi huu ya ndoa.

Lakini pia amewataka wasanii wa injili waliogeukia kufanya muziki wa kiduani kutubu na kurudi kumtukia mwenyezi mungu ikizingatiwa kuwa bado wana nafasi nyingine ya kuwaburudisha mashabiki zao .

Hata hivyo amemkataa hadharani msanii Ringtone Apoko ambaye amekuwa akijiita mwenyekiti wa muziki wa injili nchini kwa kusema kuwa sio vibaya msanii kujitawaza jina hilo lakini kwa upande wake yeye anahisi Yesu pekee ndiye anastahili kushikilia wadhfa huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *