
Watoto wa Uganda waliong’arisha video za wanamuziki mbalimbali wakubwa ikiwemo ya ‘Unforgettable’ ya French Montana wanaojulikana kama Ghetto Kids, wakutana na mshambuliaji kutoka nchini Argentina, Sergio Kun Aguero ambaye tayari amestaafu soka.
Aguero amekutana na Ghetto Kids na kupata nao burudani kidogo wakiwa katika matembezi huko nchini Qatar, zinapofanyika fainali za Kombe la Dunia 2022.
Mbali na Aguero, Ghetto Kids wakiwa bado wapo huko Qatar tayari wamekutana na mastaa wengine wakubwa Duniani, na kupitia kurasa zao za mitandao ya Kijamii wame-share picha nao.