LifeStyle

Akothee Aeleza Namna Magonjwa Yalivyobadilisha Maisha Yake

Akothee Aeleza Namna Magonjwa Yalivyobadilisha Maisha Yake

Mwanamuziki kutoka nchini Kenya, Akothee, amefunguka kuhusu mabadiliko makubwa kwenye maisha yake baada ya kugunduliwa na matatizo ya kiafya yakiwemo mashambulizi makali ya kichwa (migraine), damu kuganda, na fibroids.

Kupitia ujumbe mrefu kwenye ukurasa wake wa Instagram, Anasema hali hizo zimemlazimisha kupunguza kasi na kubadili mtazamo wake kuhusu maana ya nguvu na maisha.

Akothee amesema changamoto hizo zimemfundisha kuwa nguvu ya kweli si kupambana kila wakati, bali ni kujipa nafasi ya kupumzika na kupona. Ameeleza kuwa sasa anaheshimu mwili wake zaidi, anaepuka presha zisizo za lazima, na kutilia mkazo amani na utulivu kama tiba yake kuu.

Aidha, amewatia moyo wanawake wengine wanaopitia changamoto za kiafya kimyakimya, akisema hawapaswi kuona hali hizo kama udhaifu, bali kama safari ya mabadiliko na ukuaji.. Ameongeza kuwa sasa anaheshimu zaidi mwili wake na kuepuka presha zisizo za lazima.

Kwa ucheshi wake wa kawaida, Akothee ametaniana na wafuasi wake akisema wanaweza kumuita “Fibroids, Migraines, Bloodclot Akoth Kokeyo,” huku akisisitiza kwamba upendo wa kweli ni ule unaoonyeshwa mtu akiwa hai, na kwamba huu ni wakati wake wa kuthamini utulivu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *