Mwanamuziki Akothee amewataka mashabiki wake wajifunze kuheshimu mipaka kati ya maisha ya umaarufu na binafsi baada ya kukiri usumbufu ambao upokea kutoka kwa wafuasi wake.
Kupitia ujumbe wake wa mtandaoni, Akothee amesema kwamba kuwa mtu maarufu haimaanishi kila wakati yuko tayari kupiga picha au kutabasamu mbele ya umma.
Mwanamama huyo wa watoto sita, amesema kuwa wakati mashabiki wanapomuona kwenye maeneo ya binafsi kama vile migahawani, viwanja vya ndege, madukani au hospitalini, wanapaswa kumruhusu kuwa huru na kumpa nafasi ya faragha.
Akothee amesisitiza kwamba wakati mwingine anahitaji utulivu wa kupumzika kama binadamu wa kawaida. Hata hivyo, amewahakikishia mashabiki wake kwamba anathamini upendo wao na anafurahia kuwaona katika hafla au matamasha yake, ambako huwa tayari kupiga picha na kushirikiana nao kwa furaha.