
Album ya The Game “Drillmatic” imeuza Jumla ya nakala 25,000 kwenye wiki yake ya kwanza sokoni. Album hiyo imechumpa hadi namba 10 kwenye chart za Billboard 200.
Hii inakuwa Album ya 9 kwa The Game kuingia kwenye Top 10 ya Chart hizo za Album bora. Ni ongezeko la nakala 2,000 toka kwenye mauzo ya Album yake iliyopita “Born 2 Rap” ambayo iliuza nakala 23,000 kwenye wiki yake ya kwanza.
Wengi wanahoji juu ya mauzo haya wakisema Muziki wa The Game umeporomoka sana, kuna haja ya kubadili staili au aachane kabisa na Muziki. Una maoni gani kuhusu hili, tuachie comment yako.