
Mwimbaji wa Bongofleva Ali kiba amesema akipata nafasi ya kwenda kuonana na R. Kelly ambaye anatumikia kifungo cha miaka 30 jela atafanya hivyo.
Ali Kiba ameiambia XXL ya Clouds FM kuwa hata hivyo itakuwa ni wakati mgumu kuonana naye wakati huu wa matatizo , hivyo anaona ni bora kutuma salamu tu.
“Nikipata hiyo nafasi nitaenda kumtembelea lakini sijui nitaongea naye nini. Vitu alivyofanya mimi siwezi kuvisapoti,” amesema.
“Mimi binafsi nitaona aibu. Labda ni vizuri kutuma salamu kuliko kwenda kuonana naye,” amesema Alikiba.
Utakumbuka September 2022 Alikiba ataanza tour yake nchini Marekani baada ya kutofanya hivyo kwa miaka minne.
R Kelly katika kitabu chake, Soulacoaster: The Diary of Me, amezungumzia jinsi ulivyokuwa wakati mzuri kwake kufanya wimbo na Alikiba.
Wawili hao walikutana katika mradi wa One8 uliokutanisha wasanii wakubwa Afrika na kufanya wimbo wa pamoja unakwenda kwa jina la Hands Across The World.
Wasanii wengine walioshiriki katika mradi huo ni Amani (Kenya), Navio (Uganda), 2Face Idibia (Nigeria), 4×4 (Ghana), Fally Ipupa (DR Congo), JK (Zambia) na kundi la Movaizhaleine (Cabon