Tech news

Apple Creator Studio Yaleta Mapinduzi kwa Creators

Apple Creator Studio Yaleta Mapinduzi kwa Creators

Kampuni ya teknolojia ya Apple imezindua rasmi huduma mpya za kulipia zilizopewa jina la Apple Creator Studio, kifurushi kinacholenga kuwasaidia wabunifu wa maudhui (creators) katika nyanja mbalimbali za ubunifu wa kisasa.

Kupitia huduma hii, watumiaji wa Mac, iPhone na iPad wataweza kulipia kiasi cha shilingi 32,500 kwa mwezi, sawa na dola 12.99 za Kimarekani, na kupata matumizi ya programu kadhaa maarufu za Apple kwa bei moja ya pamoja.

Kifurushi cha Apple Creator Studio kinajumuisha programu muhimu kama Final Cut Pro, Logic Pro, Pixelmator Pro, Motion, Compressor, MainStage, pamoja na vipengele vipya vya akili bandia (AI) vilivyoongezwa kwenye apps za Keynote, Pages na Numbers. Programu hizi zinatumika sana katika uhariri wa video, utengenezaji wa muziki, graphics, pamoja na uandishi wa kitaalamu.

Apple imesema lengo la kifurushi hiki ni kuwapa creators uwezo wa kupata features za kisasa, kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na kutumia programu zote muhimu bila kulazimika kulipia kila app kivyake. Huduma hii inalenga hasa watengenezaji wa muziki, video, wabunifu wa picha na waandishi wanaotumia mifumo ya Apple.

Hatua hii ya Apple inatajwa kuwa inaweza kupunguza utegemezi wa Adobe Creative Cloud kwa baadhi ya creators, hususan wale wanaotumia Mac na iPad kama zana zao kuu za kazi. Hata hivyo, Adobe bado inaendelea kuwa na soko kubwa kutokana na wingi wa plugins, zana maalum na community yenye uzoefu mkubwa duniani kote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *