Sports news

Asaia Lasoi Ashinda Mbio za Boston Marathon

Asaia Lasoi Ashinda Mbio za Boston Marathon

Mwanariadha Isaia Lasoi kutoka Kenya alishinda katika mbio za nusu marathoni za Boston mwaka huu zilizoandaliwa nchini Marekani. Lasoi, ambaye anajivunia muda bora wa dakika 58 na sekunde 10, alishinda mbio hizo kwa saa 1 na sekunde 59, akimaliza mbele ya Santiago Catrofe wa Uruguay, ambaye alitumia muda wa saa 1 na dakika 1 na sekunde 23.

Andrea Kiptoo wa Kenya alijihakikishia nafasi ya tatu kwa muda wa saa 1 na dakika 1 na sekunde 31. Katika mbio za wanawake, Evaline Chirchir wa humu nchini alimaliza wa tatu kwa muda wa saa 1 na dakika 9 na sekunde 1.

Fantaye Belayneh wa Ethiopia alitwaa taji ya wanawake kwa saa 1 na dakika 8 na sekunde 51, akimshinda mwenzake Melknat Wudu kwa sekunde mbili tu. Makala ya mwaka huu yaliwavutia washiriki 7,000.

Mbio hizo zilikuwa za awamu ya tatu na ya mwisho mwaka huu ya shirikisho la riadha la Boston ambayo ilianza na  mbo za kilomitaa tano za Boston mwezi Aprili na na kisha mbio za kilomita 10 za Boston mwezi Juni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *