Baada ya kipindi cha miezi 11 kupita bila kuachia ngoma yoyote, msanii wa Bongofleva Aslay ameweka wazi kuwa ana njaa ya kufa mtu.
Kupitia ukurasa wake wa instagram Hitmakr huyo wa “Nyang’anya” ameweka video iliyoambatana na caption “I’m Hungry AF”
Huenda tafsiri yake ni ujio mkubwa wa kazi zake kuanzia mwaka 2022 ambapo hivi karibuni amekuwa akiacha nafasi kubwa kwenye utoaji wa kazi.
Tutegemee pia Aslay Isihaka akiisumbua Afrika, ikiwa ni tafsiri ya emoji ya dunia ambayo amekuwa akiitumia kwenye caption zake