Msanii Akothee Afunguka Kuhusu Mipango Yake ya Mazishi
Mwanamuziki kutoka Kenya, Akothee, ameibua gumzo mitandaoni baada ya kutoa tamko jipya kuhusu mipango yake ya mazishi. Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, ameeleza kuwa hataki chakula chochote kipikwe siku ya mazishi yake, akisisitiza kuwa watu wanaohudhuria wanapaswa kubeba chakula chao kutoka nyumbani badala ya kutegemea familia yake. Akothee amehoji ni vipi watu wanaweza kumudu kula kwenye mazishi, akiongeza kuwa yeyote anayetaka kula siku hiyo anapaswa kuchangia gharama mapema na kula nyumbani kwao. Mwanamama huyo, amesema wazi kuwa hafurahishwi na utamaduni wa baadhi ya watu kutumia mazishi kama fursa ya kula na kunywa badala ya kutoa heshima kwa marehemu. Kauli yake inakuja siku chache baada ya kueleza kuwa atakapoaga dunia angependa kuzikwa ndani ya saa 48, bila kujali mahali atakapofia, akisisitiza kuwa hataki mchakato wa mazishi wake ucheleweshwe.
Read More 
								 
			 
			 
			 
			 
			