Mrembo wa mitandao na mtangazaji maarufu, Azziad Nasenya, ameibua mjadala baada ya amemuanika hadharani kijana anayejulikana kama Madollar Mapesa, kufuatia madai kwamba anamdai shilingi milioni 3.
Katika sauti ya simu iliyovuja mtandaoni, Azziad alisikika akimuuliza Madollar sababu za kusambaza taarifa za uongo, akisisitiza kuwa tayari alimlipa fedha zote alizokuwa akimdai, ambazo ni jumla ya milioni 2.5.
Katika mazungumzo hayo, Madollar alisikika akipatwa na kigugumizi kabla ya kuongeza madai ya shilingi laki tano akizotaja kama interest au riba ya deni lake. Kauli hiyo ilimkasirisha Azziad ambaye alimwonya vikali akome kutumia jina lake vibaya na kueneza madai yasiyo na msingi.
Tukio hili limezua gumzo mitandaoni, huku mashabiki wengi wakimtetea Azziad na kumtaka Madollar kuthibitisha madai yake au kuomba radhi hadharani.