Entertainment

B CLASSIC AMZIMIA KIMAPENZI BABY MAMA WA MCHEKESHAJI MULAMWAH, CAROL SONNIE

B CLASSIC AMZIMIA KIMAPENZI BABY MAMA WA MCHEKESHAJI MULAMWAH, CAROL SONNIE

Waswahili wana msemo wao mmoja huwa wanasema “Penzi ni kikohozi halijifichi” msemo huu umethibitishwa na msanii b classic baada ya kukiri hadharani anamzimia kimapenzi baby mama wa mchekeshaji, Mulamwah,aitwaye Carol Sonnie.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram B classic amefunguka na kudai kwamba ameumizwa na kitendo cha mulamwah kumkimbia msichana mrembo kama sonnie ambaye kwa mujibu wake ana vigezo vyote vya kuwa mke.

Hitmaker huyo wa Mapenzi bila Pombe ametoa ya moyoni kwa kusema kwamba yuko tayari kumchukua sonnie awe mke wake ambapo ameenda mbali zaidi na kuahidi kwamba atampenda pamoja na mtoto wake kwa moyo wake wote.

Hata hivyo kauli hiyo ya B classic imeibua hisia mseto miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii ambapo wengi wanahoji msanii anatumia ishu ya mulamwah kuachana na baby mama wake kujitafutia umaarufu.

Ikumbukwe juzi kati Mulamwah aliutangaza kuachana na baby mama wake Carol Sonnie kwa sababu ambazo hakuziweka wazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *