
Wasanii wa Kundi la B2C Entertainment kutoka Uganda wametangaza kusitisha ziara yao ya muziki iliyopaswa kuanza rasmi mwezi huu wa Juni huko barani Ulaya.
Kupitia taarifa waliyochapisha kwenye mitandao yao ya kijamii wasanii wa kundi hilo kwa masikitiko makubwa wamesema wamelazimika kupiga chini show hiyo kwa sababu ambazo zipo nje ya uwezo wao.
Hata hivyo wamewaomba radhi mashabiki wao wote ambao kwa njia moja au nyingine wameathirika na uamuzi wao huo huku wakiahidi kufanya ziara nyingine kama hiyo barani Ulaya siku za mbeleni.
Utakumbuka B2C walipaswa kufanya shows zao nchini Uturuki, Ujerumani na Uingereza Juni 4, 5 na 6 mtawalia.