
Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Barnaba Classic amesema kuwa album yake ijayo itakuwa Bora kwa mwaka 2022.
Barnaba ametoa sifa hiyo juu ya album yake kupitia insta story kwenye mtandao wa Instagram, huku akieleza kuwa ameshirikiana na wasanii wengi wa ndani na nje ya Tanzania.
“Kwanza muziki nilioutumia” ameeleza Barnaba ikiwa hiyo ni sababu ya kwanza. “Nimetoa nafasi kwa new generation (vizazi vipya) kunipa mchango wa mawazo”. Sababu ya tatu Barnaba ameeleza, “Ndio album yangu ya kwanza kupata nafasi ya kushirikisha wenzangu wengi, ndani na nje ya nchi”.
Aidha, barnaba classic amedai album yake imekamilika kwa aslimia 78% na atatoa mwongozi ikishakuwa tayari.
Album hiyo inaenda kuwa album ya tano kwa mtu mzima barnaba classic tangu aanze kufanya muziki wa bongofleva miaka 20 iliyopita.