
Mchekeshaji Chris Rock ameripotiwa kuvuna pakubwa kutokana na umaarufu wa muda alioupata baada ya kupigwa kofi na mwigizaji na mwanamuziki Will Smith.
Tukio hilo lililojiri Machi 27, 2022 katika ukumbi wa maonyesho wa Dolby huko Los Angeles. Rock alikuwa jukwaani kwa ajili ya kukabidhi tuzo ya Oscar, kilichosababisha apigwe kofi ni baada ya kutania hali ya mke wa Will Smith ya kupoteza nywele kichwani.
Rock alikuwa amepanga onyesho la vichekesho katika sehemu mbalimbali ambalo amelipa jina la βEgo Death Comedy Tourβ ambalo litaanza rasmi Aprili 2 huko New Jersey nchini Marekani na ripoti mbalimbali zinaeleza kwamba viti vyote tayari vimelipiwa.
Kabla ya ziara hiyo ya mchekeshaji Chris Rock, amepanga onyesho katika ukumbi wa Wilbur huko Boston na tiketi za onyesho hilo ziliongezwa bei na kuuzwa kwa wingi zaidi.
Kampuni moja maarufu ya uuzaji tiketi za maonyesho iitwayo βTickPickβ iliandika kwenye Twitter kwamba wameuza tiketi nyingi zaidi za wanaotaka kumuona Chris Rock akichekesha kwa usiku mmoja ikilinganishwa na jumla ya tiketi ambazo waliuza kwa maonyesho yake ya mwezi mmoja uliopita.
TickPickiumeripoti kwamba mauzo ya tiketi kwa ziara hiyo ya ucheshi yamepanda mara 200, wanasema machi 28 tiketi zilinunulika zaidi baada ya tukio la chris rock kupigwa kofi huku bei zikipanda kutoka shilling elfu 5, kwa tiketi hadi elfu 39 za Kenya.