
Rapa kutoka Marekani Big Sean ametangaza rasmi kuwa ameigura lebo ya Good Music na kwa sasa ameanzisha lebo yake mpya iitwayo “FF to Def Entertainment”
Sean ametangaza hilo kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo kazi ya kwanza chini ya lebo hiyo ni EP yake mpya iitwayo ‘What You Expect’ ambayo ameshirikiana na Hit Boy.
Mwishoni mwa mwaka wa 2020 Big Sean alitangaza kuwa atajitoa kwenye lebo hiyo ya Kanye West baada ya kuachia album yake iitwayo Detroit II.
Sababu kubwa ya rapa huyo kufanya hivyo ni katika harakati za kutafuta fungu lake halali baada ya malalamiko kwamba anamdai Kanye West mamilioni ya dola.
Lebo yake mpya “FF to Def Entertainment” inafanya kazi kwa ushirikiano na Def Jam Records.