
Bruno K ni mtu mwenye moyo wa uhuruma na mara nyingi amekuwa akionyeshwa ukarimu wake kupitia vitendo kwa watu wenye uhitaji katika jamii.
Juzi kati alimchukua msanii, Oscar Bigtym (Scar) ambaye alikuwa akilala kwa vibanda huku akiuza vyuma kujikimu kimaisha.
Oscar Bigtym alikuwa moja kati ya wasanii waliokuwa wanafanya vizuri nchini uganda lakini alipoteza mweelekeo baada ya kuanza kubugia pombe kupindukia.
Bruno K alimpeleka kwenye kituo cha kurekebisha tabia na kisha akamrudisha studio kurekodi muziki. Lakini pia akatoa wito kwa wasanii wenzake akiomba msaada wa kumsaidia msanii huyo, lakini ni Pallaso na Kenneth Mugabi pekee ndio waliitikia wito wa kutoa msaada.
Sasa akiwa kwenye moja ya interview Bruno K amesikitishwa na hatua ya wasanii kukosa umoja kwenye suala la kuwasaidia wasanii wenzao ambao wamekuwa na matatizo.
Bruno K amesema licha ya Oscar kutopata msaada kutoka kwa wasanii wenzake anaamini msanii huyo ana kipaji ambacho kitampandisha tena kileleni kwa mara nyingine.
Ikumbukwe Oscar anadaiwa kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki Sheebah Karungi lakini mpaka sasa mrembo huyo hajatoa tamko lolote kuhusiana na masaibu yake.