Mwanamitindo na mshawishi wa mitandao ya kijamii, Carrol Sonnie, amefunguka kwa hasira baada ya kukerwa na kitendo cha mtumiaji maarufu wa TikTok, Shikie, kukosoa mabadiliko ya umbo lake la mwili.
Katika mfululizo wa jumbe alizozichapisha kwenye kipengele cha Instagram Stories, Carrol Sonnie ameonyesha wazi kutoridhishwa na maoni ya Shikie kuhusu ongezeko la uzito wake wa hivi karibuni, akieleza kuwa mtumiaji huyo wa Tiktok amekuwa akitoa maoni kuhusu maisha ya watu bila kujali hisia zao.
Sonnie amesisitiza kuwa ukosoaji wa aina hiyo unadhoofisha badala ya kujenga, na unaweza kusababisha madhara makubwa kwa afya ya kiakili ya mtu.
Mrembo huyo, ambaye pia anadaiwa kuwa mjamzito, ameongeza kuwa watu maarufu, licha ya kuwa katika macho ya umma, bado wana hisia na wanastahili kuheshimiwa kama wengine.