
Chama cha Mavampaya (Vampire’s) kimetoa onyo kwa msanii Machine Gun Kelly na mkewe Megan Fox kufuatia wawili hao kuendelea kujinadi kwenye mahojiano mbali mbali kwamba kila mmoja huwa anakunywa damu ya mwenzake.
Belfazaa Ashantison, mwanzilishi mwenza wa Chama cha The New Orleans Vampire Association (NOVA) amesema Machine Gun Kelly na Megan Fox wanapaswa kuchukua tahadhari kabla ya kunywa damu hizo ikiwemo kufanya vipimo kubaini magonjwa kama HIV, Malaria, Syphilis, Brucellosis na mengine makubwa.
Aidha wamekazia kwamba Vampire hufanya utafiti wa kutosha angalau kwa miezi 6 ili kumfahamu mtu ambaye atakuwa akinywa damu yake bila wasiwasi na hufanya vipimo kila baada ya miezi mitatu ili kujiridhisha tena.