LifeStyle

Charisma Afunguka Kuhusu Ulevi Uliomfikisha Kwenye Hatari ya Kujitoa Uhai

Charisma Afunguka Kuhusu Ulevi Uliomfikisha Kwenye Hatari ya Kujitoa Uhai

Msanii wa muziki kutoka Kenya, Charisma, amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu changamoto alizopitia kutokana na matumizi ya pombe kupindukia.

Akipiga stori na Iko Nini Podcast, msanii huyo ameeleza kuwa hali hiyo ilimfikisha kwenye msongo wa mawazo mkubwa kiasi cha kufikiria kujiua kwa kujinyonga akitumia kamba. Katika tukio hilo, baba na ndugu yake waliingilia kati na kumuokoa akiwa kwenye jaribu hilo.

Charisma amesema kuwa maumivu aliyoyapitia na kuona familia yake ikilia na kuomba kwa ajili yake vilimfanya achague kubadilika. Kwa sasa, msanii huyo ameanza ukurasa mpya wa maisha, akilenga muziki na familia kama nguzo za matumaini na uponyaji.

Hata hivyo, ameahidi kutumia jukwaa lake kuelimisha na kuhamasisha vijana dhidi ya matumizi ya pombe kupita kiasi, akisisitiza kuwa pombe si suluhisho bali ni njia ya kuangamiza ndoto na maisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *