
Nyota wa muziki nchini Uganda Cindy Sanyu amesitisha maombi ya kutumbuiza kwenye matamasha ya jukwaani akisema kuwa hayuko katika hali nzuri ya kuwaburudisha mashabiki wake kutokana na uja uzito wake.
Msanii huyo maarufu wa muziki wa dancehall amesema amekuwa akipokea simu za kimataifa kwa ajili ya kutumbuiza kwenye matamasha ya muziki lakini amehamua kusitisha maombi yote ya matamasha kwa sababu hataki kuwaangusha mashabiki zake ikizingatiwa kuwa anaelekea kujifungua.
Hata hivyo Cindy Sanyu ambaye kwa sasa ana umri miaka 36 anatarajia kumpata mtoto wake wa pili na mchumba wake wa Prynce Joel Atiku ambaye walianzisha mahusiano yao mwanzoni mwa mwaka wa 2020.