Gossip

Claudia Naisabwa Awatolea Uvivu Wakosoaji Baada ya Birthday Wishlist ya Sh12 Milioni

Claudia Naisabwa Awatolea Uvivu Wakosoaji Baada ya Birthday Wishlist ya Sh12 Milioni

Mtangazaji wa radio nchini Kenya, Claudia Naisabwa, ameibua gumzo mitandaoni baada ya kuwatolea uvivu wakosoaji waliomshambulia kwa kushiriki orodha ya zawadi anazotamani kupata kwa siku yake ya kuzaliwa.

Akiwa hewani Nation FM, Claudia amesema wazi kuwa watu aliowaalika kwenye sherehe yake si watu wa njaa bali ni watu wenye pesa, na kusisitiza kuwa asiyekuwa na hela hana sababu ya kuzungumzia maisha yake.

Mrembo huyo amesisitiza kuwa moja ya zawadi kuu anazozitaka ni Porsche Cayenne, akiongeza kuwa anajua hadhira yake na hategemei mtu asiye na uwezo kujihusisha na mipango yake ya sherehe.

Mjadala huu uliibuka baada ya Claudia kuposti kwenye Instagram “birthday wish list” yenye thamani ya zaidi ya Sh12 milioni, ikijumuisha bidhaa ghali kama MacBook Pro M4, simu mpya ya iPhone 16 Pro Max, saa ya Apple Watch Series 10, vito vya Swarovski, manukato ya Versace, begi la ALDO Celestica, na gauni maalum kutoka kwa mbunifu Kanazie. Aidha, aliongeza safari ya kwenda Malaysia na mchango wa pesa taslimu kama sehemu ya matakwa yake.

Kwa maelezo yake, Claudia alisema orodha hiyo ilikuwa mwongozo kwa wageni wake kuhusu zawadi anazozitamani, huku akibakiza siku nane kuelekea sherehe yake ya kuzaliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *