LifeStyle

Corazon Kwamboka ashauri wanawake kuwa makini na kalori za ugali

Corazon Kwamboka ashauri wanawake kuwa makini na kalori za ugali

Mwanamitindo na wakili kutoka Kenya, Corazon Kwamboka amewataka wanawake wanaotaka kudumisha umbo zuri na mwili wenye afya kuwa makini na ulaji wa ugali kupita kiasi.

Kupitia mitandao ya kijamii, Corazon ameeleza kuwa ingawa ugali ni chakula muhimu kwa Wakenya wengi, ulaji wake wa mara kwa mara unaweza kuchangia ongezeko la uzito kutokana na wingi wa kalori

Mrembo huyo, amesema kuwa yeye binafsi bado hula ugali, lakini amepunguza ulaji wake hadi mara moja au mbili tu kwa mwezi ili kudhibiti kalori anazozipata.

Lakini pia amefichua mpango wake rahisi wa mlo wa kupunguza mafuta mwilini, akisema anafuata mpango wa mlo wenye protini nyingi unaolenga kupunguza mafuta bila kupoteza umbo au nguvu za mwili. Amesema mpango huo ni rahisi na hauna ugumu wowote.

Kwa mujibu wake, mpango huo unahusisha aina tatu tu za protini, aina tatu za wanga wenye wanga kidogo (starches), na mboga rahisi ambazo huzirudia kwa wiki nzima. Corazon amesema lengo lake ni kudumisha uwiano wa lishe bora bila kutumia vyakula vingi vya gharama au visivyopatikana kwa urahisi.

Ujumbe wa Corazon umeibua mijadala mitandaoni, baadhi ya wafuasi wakikubaliana naye kuwa lishe yenye uwiano na nidhamu ya kula ni muhimu kwa kudumisha afya, huku wengine wakimtetea ugali kama chakula cha jadi kisichopaswa kuepukwa kabisa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *