
Mkali wa muziki wa Reggaeton Duniani, msanii Daddy Yankee ametangaza rasmi kustaafu muziki, ikiwa ni miaka 28 tangu aingie kwenye muziki.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Gasolina” kutoka Puerto Rico, ametoa taarifa hiyo kupitia website yake ambapo amesema kwa sasa anapumzika akihitaji kujikita zaidi kwenye masuala yake binafsi.
Lakini pia amesema mwaka huu ataachia album yake ya mwisho iitwayo “Legendaddy” na kisha atafanya ziara na kisha atafanya ziara ya kuwaaga mashabiki zake.