
Kwa kawaida, kwenye kila sherehe au matatizo, suala la michango huwa ni kigugumizi kikubwa kwa watu wengi duniani.
Hii imekua tofauti kidogo kwa Staa wa muziki kutoka nchini Nigeria Davido ambaye amekuja na mbinu tofauti ya kupata zawadi kutoka kwa marafiki zake kwenye siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.
Davido ameamua kutumia mitandao ya kijamii kupitia kurusa zake za twitter na instagram kuchangisha kiasi cha fedha kuanzia shilling laki 2 kutoka kwa marafiki zake haswa mastaa wakubwa wa muziki barani africa pamoja na wafanyabiashara.
Kwa wasanii amewataja Diamond Platnumz, Ckay, Focalistic, Patoranking, Tiwa Savage, Don Jazzy, Olamide na wengine kibao ambapo mpaka sasa kuna baadhi ya mastaa ambao wamemchangia pesa. Kupitia account yake ya bank mpaka sasa amepokea zaidi na shilling milioni 18.6.
Davido amefanya hivyo kuelekea siku ya kuzaliwa kwake ambayo ni novemba 21 na lengo lake ni kufikisha shillingi milioni 27.