
Mwanamuziki kutoka Nigeria Davido na menejimenti yake wametoa taarifa kwa umma, wamesema ule mchakato wa kusaidia watoto yatima umekamilika ambapo kiasi cha shilllingi million 68 za Kenya zimekabidhiwa kwa vituo 292 vya watoto yatima nchini kwao.
Mwezi Novemba mwaka jana Davido alipokea kiasi cha shilling millioni 54 kutoka kwa marafiki zake na wadau ambao walichangisha kupitia mitandao ya kijamii kwenye siku yake ya kuzaliwa.
Davido aliahidi kiasi hicho cha fedha atakipeleka kwa watoto yatima na akaongeza shillingi millioni 13 kutoka kwenye mfuko wake, hivyo kukafikisha jumla ya shillingi millioni 68.