
Mwaka 2023 umeanza vyema kwa Davido baada kushinda tuzo 5 za AFRIMA (All Africa Music Awards) 2023 zilizotolewa usiku wa kuamkia leo huko Dakar, Senegal.
Davido amebeba tuzo ya (Best Male Arist African Inspirational Music) kupitia wimbo wake StandStrong.
Tuzo ya PILI ni (Best Duo/Group in African Electro) kupitia wimbo wake ChampionSound aliomshirikisha Focalistic na Tuzo yake ya TATU ni (Best Act in the Diaspora Male) kupitia wimbo Who’sTrue alioshirikishwa na Tion Wayne.
Nyota huyo ambaye alifunga mwaka 2022 kwa kutoa performance kwenye fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar, tuzo yake ya NNE aliyoshinda ni (Best African Collaboration) kupitia wimbo wake ChampionSound aliomshirikisha Focalistic na ya TANO ni (Best Duo/ Group in African Pop) kupitia wimbo High alioshirikishwa na msanii Adekunle Gold.
Wakali wengine waliobeba tuzo kwenye usiku huo ni pamoja na Wizkid, Asake, Adekunle Gold.