
Mwanamuziki kutoka Nigeria davido amejikuta akilipa zaidi ya shilling million 42 za Kenya kama faini baada ya kuzidisha muda katika show yake iliyofanyika juzi kati katika uwanja maarufu nchini uingereza wa O2 Arena.
Show ya Davido ilipaswa kuisha saa tano kamili usiku ila msanii huyo alitumbuiza hadi saa saa tano na dakika 34 huku akisema hajali kuhusu faini hiyo ambayo inasema kuwa kama msanii atazidisha muda wa kutumbuiza atatakiwa kulipa shilling million 1.2 za Kenya kwa kila dakika.
Hii si mara ya kwanza kwa wasanii kulipishwa faini hizo kubwa kwani mwaka 2013, Msanii justin bieber alijikuta akilipa faini ya shilling million 37.2 za kenya baada ya kuzidisha dakika 30 kwenye ukumbi huo.