
Staa wa muziki kutoka Nigeria Davido anazidi kuongeza list ya magari ya kifahari anayoyamiliki kwenye eneo la kuegesha magari nyumbani kwake mara baada ya kuongeza gari lingine la thamani aina ya Mercedes Maybach GLS 600.
Unaambiwa ndinga hiyo mpya aina ya Mercedez Maybach GLS 600 ya Mwaka 2022 inatajwa kuwa na thamani ya $ 300K ambazo ni takribani shilling Milioni 34.2 kwa pesa ya Kenya huku akitarajia kupokea ndinga yake nyingine aina ya Lamborghini itakayotua Nigeria kutoka Dubai.