
Staa wa muziki kutoka Nigeria Davido amewatolea uvivu watu wanaopenda kuhusisha familia yake haswa watoto wake kwenye skendo zisizo na msingi kwa kueleza kuwa ni heri wamtaje kwenye skendo hizo badala ya kuwahusisha watoto wake.
Davido ameitoa kauli hiyo ambayo alikusudia kumjibu shabiki ambaye alimuambia kupitia mtandao wa twitter kuwa sio Baba halali wa mtoto wake wa kiume “Ifeanyi” ambaye alipata na Chioma. Shabiki huyo alimchana Davido kuwa mtoto huyo baba yake mzazi ni msanii Peruzzi.
Ikumbukwe msanii Peruzzi aliwahi kuhusishwa kuwa na mahusiano na Baby Mama huyo wa Davido, mwanadada Chioma.