Entertainment

DAVIDO AMTAMBULISHA MTOTO ALIYEZAA NA MREMBO WA ENGLAND LARISSA LONDON

DAVIDO AMTAMBULISHA MTOTO ALIYEZAA NA MREMBO WA ENGLAND LARISSA LONDON

Kwa mara ya kwanza mwimbaji Davido ameonekana hadharani na mtoto wake wa miaka miwili, Dawson ambaye alizaa na Makeup artist Larissa London mwenye makazi yake nchini Uingereza.

Davido ambaye yupo nchini Uingereza alipata nafasi ya kuhudhuria ibada Jana Jumapili (August 7) akiwa mtoto wake huyo wa Kiume. Kulikuwepo taarifa kuwa ni mwanaye lakini tofauti na watoto wengine, Davido hakuwahi kuonekana na Dawson hadharani.

Mkali huyo wa Nigeria ana watoto wanne Imade, Hailey, Ifeanyi na Dawson toka kwa Wanawake wanne tofauti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *