Entertainment

Familia ya Msanii Shalkido Yaomba Msaada Kukamilisha Gharama za Matibabu

Familia ya Msanii Shalkido Yaomba Msaada Kukamilisha Gharama za Matibabu

Familia ya marehemu msanii Shalkido imeomba msaada wa shilingi 147,000 ili kukamilisha gharama za matibabu aliyopatiwa kabla ya kufariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa ndugu wa karibu, Shalkido alipata ajali mbaya ya barabarani usiku wa kuamkia jana na alikimbizwa hospitalini mara moja kwa ajili ya matibabu. Hata hivyo, juhudi za madaktari za kuokoa maisha yake hazikufaulu.

Familia imetoa wito kwa marafiki, mashabiki na wadau wa muziki kujitokeza kwa hali na mali ili kusaidia kufanikisha malipo ya deni la hospitali na maandalizi ya mazishi. Mchango unaweza kutumwa kupitia Mpesa namba 0116202762 (Stephen Mungai Muthoni).

Shalkido, ambaye aliwahi kujipatia umaarufu kupitia muziki wa miondoko ya Gengetone na kundi la Sailors Gang, alikuwa akitambulika kama msanii mwenye kipaji na mchango mkubwa katika tasnia ya muziki nchini Kenya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *