Familia ya msanii wa Gengetone marehemu Shalkido, imethibitisha kuwa mazishi yake yatafanyika siku ya Alhamisi, Oktoba 16, nyumbani kwao eneo la Kimbo Matangi.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Oga Obinna kwa niaba ya familia, mashabiki na marafiki wameombwa kusaidia maandalizi ya mazishi kupitia nambari ya paybill 8030444 (Akaunti: Shalkido Gacucu).
Shalkido alifariki juzi kati katika ajali mbaya ya barabarani, tukio lililowaacha mashabiki na wasanii wenzake wakiwa na majonzi makubwa.
Marehemu Shalkido alijulikana kwa mchango wake mkubwa katika muziki wa Gengetone kupitia kundi la Sailors Gang, akiwa miongoni mwa wasanii waliotoa ladha mpya katika muziki wa vijana nchini Kenya.