Gossip

Fik Fameica: “Hakuna Mwanamke Anayeweza Kunitawala”

Fik Fameica: “Hakuna Mwanamke Anayeweza Kunitawala”

Msanii maarufu wa muziki wa Hip Hop kutoka Uganda, Fik Fameica, amezungumza wazi kuhusu hulka yake ya kuwa mtu mpole na mwenye heshima, lakini akasisitiza kuwa hawezi kuruhusu watu kumchukulia poa au kumdharau kwa sababu ya unyenyekevu wake.

Akizungumza katika mahojiano ya hivi karibuni, Fik alifunguka kuhusu mitazamo ya watu wengi kumchukulia kama mtu mnyonge kwa sababu ya tabia yake ya utulivu, akieleza kuwa upole wake usichukuliwe kama udhaifu hasa katika mahusiano ya kimapenzi. Fik Fameica alisema kuwa licha ya kuwa na tabia ya utulivu na kujiheshimu, amejifunza kuwa katika maisha na tasnia ya muziki, ni muhimu pia kujua kuweka mipaka.

“Nimekuwa mtu mpole tangu nikiwa mdogo. Napenda kuwa na heshima kwa kila mtu, lakini hiyo haimaanishi kwamba watu waniingilie au kunidharau. Watu wengine wakiona uko humble, wanadhani wanaweza kukupanda kichwani. Mimi si mtu wa fujo, lakini naweza kusimama imara linapokuja suala la staha. Siwezi ruhusu mwanamke yeyote kuniongoza kama hana heshima na mipaka,” alisema Fik Fameica kwa msisitizo.

Kauli hiyo imewagawa mashabiki mitandaoni; baadhi wakimpongeza kwa msimamo wake wa kiume na kujitambua, huku wengine wakiona kama ni kauli yenye kiburi dhidi ya wanawake. Hata hivyo, Fik alisisitiza kuwa anathamini wanawake lakini pia anahitaji heshima ya kweli na si udhibiti wa kihisia au tabia za kuonea.

Mashabiki wake wengi wamepongeza mtazamo wake huo, wakisema kuwa ujumbe wake unatoa funzo kwa vijana kuwa na unyenyekevu lakini pia kujua thamani yao na kutoruhusu kutumiwa vibaya.

Fik Fameica, ambaye amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na hits kama Mafia,” “My Property” na “Buligita,” ameendelea kuwa mfano wa msanii anayejali nidhamu na maadili, huku akipaza sauti juu ya umuhimu wa kujitambua na kujithamini.