Entertainment

GRAMMY WARIDHIA OMBI LA DRAKE KUJIONDOA KWENYE TUZO HIZO 2022

GRAMMY WARIDHIA OMBI LA DRAKE KUJIONDOA KWENYE TUZO HIZO 2022

Hatimaye teuzi mbili za rapa Drake za tuzo za Grammy kwa mwaka 2022 zimeondolewa kwenye tovuti rasmi.

Kwa mujibu wa taarifa, uamuzi huo umefikia kutokana na ombi la Drake na uongozi wake.

Chanzo kotoka Recording Academy kimeiambia Newsbeat kwamba, Academy ilichagua kuheshimu matakwa yake.

Hata hivyo sababu za hilo bado hazijafahamika, na wawakilishi wa rapa huyo bado hawajajibu ombi la kutoa maoni.

Kwenye tovuti rasmi ya Grammy, inaeleza kuwa uteuzi huo umeondolewa, na hakuna mbadala, ikimaanisha kuwa upigaji kura kwa makundi hayo mawili utaendelea na wateule wanne pekee.

Drake alikuwa mmoja wa walioteuliwa kuwania Albamu Bora ya Rap, ya Certified Lover Boy, na Wimbo Bora wa Rap, kupitia singo iitwayo Way 2 Sexy.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *